SIMBA SC 5-1 PAMBA JIJI FC, REKODI ZIPO NAMNA HII

MECHI ya Simba SC 5-1 Pamba Jiji FC iliyochezwa Uwanja wa KMC Complex ilishuhudiwa ikikusanya jumla ya mabao sita huku hat trick ikipatikana kutoka kwa kiungo mshambuliaji Jean Ahoua ambaye anafikisha mabao 15 ndani ya ligi msimu wa 2024/25.

Kuna rekodi ambazo ziliandikwa Mei 8 2025 na wachezaji uwanjani kwa kila mmoja kutimiza majukumu yake katika kutafuta pointi tatu ambazo zilikwenda Msimbazi, hapa tunakuletea baadhi ya rekodi za mchezo namna zilivyokuwa:-

Moussa Camara

Alianza langoni akiokoa hatari dakika ya 25, 41, 87 alitunguliwa bao moja na Mathew Momanyi dakika ya 86 ndani ya 18.

Jean Ahoua

Kiungo mshambuliaji wa Simba SC alianza kikosi cha kwanza, alipiga faulo dakika ya 8, 27, 27, 36, 47 alipoteza mpira dakika ya 2, 11. Ni dakika ya 8, 15, 34, 36, 47 alipiga mashuti ambayo yalilenga lango dakika ya 10 alipiga shuti ambalo halikulenga lango.

Alipachika mabao matatu, dakika ya 15 kwa pigo la penati, dakika ya 36 kwa pigo la faulo na dakika ya 47 kwa pigo la kichwa akitumia pasi ya Ellie Mpanzu. Alikosa nafasi za kufunga dakika ya 23, 45. Alikomba dakika 54 Nouma aliingia.

Leonel Ateba

Alipiga mashuti ambayo yalilenga lango dakika ya 19, 23, 70, 79, 84, alitupia mabao dakika ya 79 na 84. Alichezewa faulo dakika ya 45.

Joshua Mutale

Alipiga kona dakika ya 12, 13, alichezewa faulo dakika ya 14, 35, 45, 49, alicheza faulo dakika ya 60. Alikomba dakika 70 nafasi yake ilichukuliwa na Ladack Chasambi.

 Ellie Mpanzu

Alichezewa faulo dakika ya 7, 23, 64, 71alipiga mashuti ambayo yalilenga lango dakika ya 67, 63 alipoteza pasi dakika ya 10, 23 alitoa pasi ya bao kwa Ahoua dakika ya 47 akitumia mguu wa kushoto.

Zimbwe

Mohamed Hussen Zimbwe Jr alianza kikosi cha kwanza na alipewa jukumu la kurusha dakika ya 5, alipiga krosi dakika ya 18 aliokoa hatari dakika ya 3, alicheza faulo dakika ya 40, 41.

Okejapha

Ni dakika ya 32, 38, 41, 59, 68 alitembeza mikato ya kimyakimya kwa wapinzani Pamba Jiji.

Hamza Jr

Alicheza faulo dakika ya 39, 45 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 45, aliokoa hatari dakika ya 4. 19 alikomba dakika 45 nafasi yake ilichukuliwa na Che Malone.

Shomari Kapombe

Beki huyu alichezewa faulo dakika ya 27, alicheza faulo dakika ya 30 alipiga faulo dakika ya 11 alikomba dakika 54 nafasi yake ilichukuliwa na Kibu Dennis.

Ngoma

Fabrince Ngoma alikomba dakika 54 nafasi yake ilichukuliwa na Mavambo ambaye alitoa pasi ya bao kwa Ateba dakika ya 79.

Hawa hapa Pamba Jiji

Mohamed Camara

Kipa wa Pamba Jiji aliokoa hatari dakika ya 3, 8, 34, 41, 63 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 45 na alikomba dakika zote 90.

Zabona Mayombya

Alicheza faulo dakika ya 14 iliyosababisha penati kwa Simba, alichezewa faulo dakika ya 38, alikomba dakika 67 nafasi yake ilichukuliwa na Hamad Majimengi ambaye alitoa pasi ya bao dakika ya 86 kwa Mathew na alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 90 na mwamuzi Shomari Lawi.

Mathew Teqisi

Nyota huyu alikutwa kwenye mtego wa kuotea dakika ya 25, 33 alicheza faulo dakika ya 17, 45 alichezewa faulo dakika ya 39, 41 alifunga bao moja dakika ya 86.

Shashir Nahimana

Alicheza faulo dakika ya 38, 64 alionyeshwa kadi ya njano dakika ya 64.

Yonta Camara

Nyota huyu alichezewa faulo dakika ya 45, 52, 59.

Deus Kaseke

Kaseke alianzia benchi na aliingia dakika ya 67, alichezewa faulo dakika ya 70 na Chamou,dakika ya 74.

Dakika za nyongeza

Kipindi cha kwanza ziliongezwa dakika 4 na kipindi cha pili ziliongezwa dakika 7.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.