ORODHA YA TIMU AMBAZO ZIMEPATA PENATI NYINGI BONGO

LIGI Kuu Tanzania Bara msimu wa 2024/25 inaendelea huku ushindani ukiwa mkubwa huku kila timu ikipambania malengo yake ndani ya dakika 90.

Kwenye eneo la utupiaji wachezaji wanaendelea kutimiza majukumu yao huku kiungo mshambuliaji Jean Ahoua akiwa namba moja akiwa katupia mabao 15 na pasi 7 za mabao.

Ni Yanga SC inaongoza kwa timu yenye mabao mengi ambayo ni 68 ikiwa na pointi 70 nafasi ya kwanza inafuatiwa na Simba SC nafasi ya pili ikiwa na pointi 66.

Hapa tunakuletea orodha ya timu zilizopata idadi nyingi ya mikwaju ya penalti ndani ya uwanja namna hii:-

Simba SC 13

Ipo nafasi ya pili kwenye msimamo safu ya ushambuliaji ikiwa imetupia mabao 68 kibindoni.

Singida Black Stars  8

Ni namba mbili kwenye msimamo ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 53 baada ya kucheza mechi 27, safu ya ushambuliaji imetupia mabao 40.

Mwendo wa 7/7

Mashujaa – 7- Kwenye msimamo ipo nafasi ya 10 baada ya kucheza mechi 27 kibindoni ina pointi 30, safu ya ushambuliaji imetupia mabao 27.

Yanga-7- Ni vinara kwenye ligi wakiwa na pointi 70 baada ya mechi 26.

Namungo FC- 7- Kwenye msimamo nafasi ya 9 ikiwa na pointi 30 safu ya ushambuliaji imetupia mabao 23.

Mwendo wa 5/5

Dodoma Jiji-5- Mechi 27 imecheza ikiwa na pointi 34 safu ya ushambuliaji imetupia mabao 30.

Tabora United-5- Ni nafasi ya tano kwenye msimamo ikiwa na pointi 37, safu ya ushambuliaji imetupia mabao 30.

JKT Tanzania-5- Kwenye msimamo nafasi ya 7 ikiwa na pointi 32, safu ya ushambuliaji imetupia mabao 24.

Coastal Union-5- Kwenye msimamo nafasi ya 8 ina pointi 31, safu ya ushambuliaji imetupia mabao 23.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.