KIUNGO MGUMU AREJEA KIKOSI YANGA

 KHALID Aucho kiungo wa Yanga amerejea uwanja wa mazoezi baada ya kuwa nje kwa muda alipopata maumivu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Coastal Union ya Tanga.

Ilikuwa ni Aprili 7 2025 Aucho aliumia alishindwa kukomba dakika 90 aliishia dakika ya 45 ambapo nafasi yake ilichukuliwa na kiungo Mudathir Yahya.

Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa KMC Complex baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 3-0 Coastal Union.

Alikosekana kwenye mechi zilizofuata kutokana na kuendelea kupewa matibabu ilikuwa mchezo dhidi ya Azam FC uliochezwa Uwanja wa Azam Complex na mchezo dhidi ya Fountain Gate uliochezwa Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa.

Katika Dar Dabi Aprili 10 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 1-2 Yanga mabao ya Pacome na Prince Dube kwa Yanga na Lusajo kwa Azam FC.

Mchezo wa pili ilikuwa dhidi ya Fountain Gate Aprili 21 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Fountain Gate 0-4 Yanga pointi sita ndani ya dakika 180 ambazo alikosekana zote ilikuwa ni mali ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi.

Ameanza mazoezi na wachezaji wenzake ikiwa ni maandalizi kuelekea mchezo ujao wa ligi dhidi ya Namungo FC unaotarajiwa kuchezwa Mei 13 2025 Uwanja wa KMC Complex.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.