SIMBA SC KAMILI KWA KARIAKOO DABI

UONGOZI wa Simba SC umeweka wazi kuwa upo tayari kwa mchezo wa Kariakoo Dabi ambao unatarajiwa kuchezwa Juni 15 2025.

Awali mchezo huo ulipangwa kuchezwa Machi 8 2025 ukayeyuka baada ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, (TBLB) kubainisha kuwa mchezo huo namba 184 umeahirishwa na utapagiwa tarehe nyingine.

Yanga SC ilibainisha kuwa mchezo huo wao hawatacheza na walipeleka kesi CAS ambapo Mei 5 2025 walitoa taarifa kuwa wamepokea majibu ya CAS huku wakitakiwa kurejea mamlaka ya ndani ambayo hawana imani nayo hivyo msimamo wao ni kuwa hawatacheza mchezo huo.

Taarifa kutoka TPLB imetangaza ratiba ya mechi za ligi kwa ajili ya kukamilisha mzungungo wa pili 2024/25 huku wakiupangia mchezo wa Kariakoo Dabi Yanga SC na Simba SC Juni 15 2025.

Mei 5 2025, Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba aliweka wazi kuwa wapo tayari kwa mchezo huo muda wowote ukipangwa.

“Sisi hatuna tatizo muda wowote tupo tayari wakipanga ratiba wakitupa tarehe kama ambavyo wamesema mapema iwezekenavyo tutapeleka timu, kikubwa tupo tayari na timu yetu ni imara.”

 

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.