NGOMA AFICHUA SIRI YA BAO LA USHINDI

FABRINCE Ngoma kiungo mshambuliaji wa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids amesema kuwa siri ya kufunga bao la ushindi dhidi ya JKT Tanzania ni kutimiza majukumu ya timu kwenye msako wa pointi tatu.

Mei 2 2025 Simba ilikuwa na kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Mashujaa FC ambapo walipata ushindi wa mabao 2-1 na Ngoma alikosekana kwenye mchezo huo pamoja na kiungo Jean Ahoua.

Mei 5 2025 Simba SC ilikuwa Uwanja wa Isahmuyo walipata ushindi wa bao 1-0 ambalo lilifungwa na Ngoma dakika ya 45 akiwa ndani ya 18 akimalizia pasi ya Steven Mukwala.

Baada ya dakika 90 Ngoma alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo huo na Simba ilikomba pointi tatu mazima kwenye mchezo wa pili ndani ya dakika 180 kwa ushindi wa bao mojamoja.

Ngoma amesema kuwa walikuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu na waliingia uwanjani kwa tahadhari ili kupata matokeo mazuri.

“Tunatambua kwamba ushindani ni mkubwa jambo ambalo linafanya tufanye kazi kubwa kusaka pointi tatu ndani ya uwanja, tupo tayari na tunafuata maelekezo ya benchi la ufundi kwenye mechi zetu zote ambazo tunacheza ili kupata matokeo mazuri.”

Simba SC kwenye msimamo wa ligi ni namba mbili ikiwa na pointi 63 baada ya mechi 24 JKT Tanzania ni namba 7 kwenye msimamo ikiwa na pointi 32 baada ya kucheza mechi 27.