DICKSON Job beki chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miloud Hamdi anatajwa kuwa ameitwa mezani ili kujadili suala la kuongeza mkataba wake mpya.
Beki huyo amekuwa kwenye ubora wake kwenye mechi ambazo anacheza jambo ambalo linaongeza thamani yake kuzidi kupanda.
Taarifa zinaeleza kuwa mara baada ya Muungano Cup 2025 kugota mwisho na Yanga SC kutwaa taji hilo tayari wamefungua ukurasa mpya wa mazungumzo na beki huyo ili aongeze mkataba mwingine kuendelea kuwa ndani ya Jangwani.
Mkataba wa Job unatarajiwa kugota mwisho msimu utakapotamatika 2024/25 huku ikitajwa kwamba kuna timu zaidi ya mbili ambazo zinahitaji saini ya Job.
Ikumbukwe kwamba Job aliibuka Jangwani akitokea ndani ya Mtibwa Sugar ambayo ilishuka daraja na kucheza Championship na sasa 2024/25 imerejea na itakuwa ndani ya ligi msimu mpya wa 2025/26 ikitumia Uwanja wa Manungu kwa mechi za nyumbani.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.