VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika, Yanga SC tofauti yao kwenye pointi na Simba SC ni pointi 10.
Ikumbukwe kwamba wababe hawa wawili hawajakutana mzunguko wa pili baada ya mchezo wao kuyeyuka Machi 8 2025 unatarajiwa kupangiwa tarehe na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara.
Sababu ambazo zilisababisha mchezo wao usipangiwe tarehe ni baada ya Yanga SC kukata rufaa kwenye mahakama ya kimataifa ya usuluhishi wa michezo, (CAS) kesi hiyo ilipewa namba CAS 2025/A/11298 ambapo Yanga ilifungua shtaka dhidi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, (TFF) kuhusiana na mchezo namba 184 wa ligi, Yanga vs Simba.
Yanga SC iliomba mechi hiyo isipangiwe tarehe mpaka litakapotolewa uamuzi ambapo walalamikiwa wengine walikuwa ni Simba, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB). CAS imetupa rufani hiyo ya Yanga SC hivyo TPLB inaendelea na maandalizi yake kwa ajili ya kuhitimisha msimu wa 2024/25 ambapo mchezo huo utatangazwa hivi karibuni tarehe taarifa hiyo ilitolewa Mei Mosi 2025.
Ndani ya uwanja Yanga imetupia jumla ya mabao 68 baada ya mechi 26 huku Simba ikiwa imetupia mabao 54 baada ya mechi 23 tofauti kwenye mabao ni 14 ambapo Yanga SC ni vinara kwenye eneo la utupiaji.
Kwa upande wa pointi, Yanga ana pointi 70 kibindoni baada ya mechi 26 huku Simba ikiwa na pointi 60 baada ya mechi 23 napo tofauti yao ni 10.
Simba ina mechi tatu mkononi kuwafikia Yanga SC kituo kinachofuata kwa mnyama ni Mei 5 2025 itakuwa dhidi ya JKT Tanzania, Uwanja wa Ishamuyo.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.