SIMBA SC ni timu namba moja kupata penalti ndani ya Ligi Kuu Bara ikiwa imepata jumla ya penalti 12 msimu wa 2024/25 katika Ligi Kuu Tanzania Bara.
Penalti mbili ambazo wamezipata dhidi ya Mashujaa FC Mei 2 2025 zote zikifungwa na Leonel Ateba katika ushindi wa mabao 2-1 Mashujaa FC zinamfanya Ateba kufikisha jumla ya penalti 7 zakupiga akipata sita na kukosa moja huku tano zikifungwa na Jean Ahoua.
Ubao wa Uwanja wa KMC Complex baada ya dakika 90 ulisoma Simba SC 2-1 Mashujaa na bao la Mashujaa likifungwa na Jaffary Kibaya dakika ya 6.
Bao la Kibaya lilidumu mpaka dakika ya 65 ambapo Simba ilipata bao kupitia kwa Ateba ambaye alifunga kwa mkwaju wa penati na dakika ya 90 alifunga bao la pili la ushindi kwa mkwaju wa penati.
Mwamuzi wa kati alikuwa ni Kefa Kayombo ambaye alikuwa akisimamia sheria 17 za mpira na kipindi cha pili alimuonyesha kadi nyekundu kipa namba moja wa Mashujaa Patrick Munthali kwa kuwa alionyesha kadi mbili za njano kwenye mchezo huo ya kwanza ilikuwa dakika ya 50 na ile ya pili ilikuwa dakika ya 78.
Simba SC inafikisha pointi 60 ikiwa nafasi ya pili kwenye msimamo na Mashujaa nafasi ya 10 pointi 30 kibindoni.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.