YANGA YAANGUKIA PUA CAS, KARIAKOO DERBY IPO PALE PALE

MAHAKAMA ya Kimataifa ya Usuluhishi wa Michezo (CAS) imetupa rufani ya klabu ya Yanga yenye kumbukumbu namba CAS 2025/A/11298 ambayo klabu hiyo iliifungua dhidi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuhusiana na mchezo wa Ligi Kuu wa Derby ya Kariakoo kati ya Yanga Sc dhidi ya Simba Sc ulioahirishwa.

Taarifa ya Shirikisho la soka Tanzania (TFF) iliyotolewa leo Mei 01, 2025 imeeleza kuwa walalamikiwa wengine katika shauri hilo ambapo pamoja na mengine, klabu ya Yanga iliomba mechi hiyo isipangiwe tarehe mpaka litakapotolewa uamuzi, ni Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB), na klabu ya Simba.

Kutokana na uamuzi huo wa CAS, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania inaendelea na maandalizi yake ya kuhitimisha msimu wa Ligi Kuu ya NBC 2024/2025 na kufanya maboresho ya ratiba ya Ligi (ukiwemo mchezo namba 184 Young Africans vs Simba SC) kisha kutangaza ratiba mpya mapema iwezekanavyo.