SIMBA KWENYE MSAKO WA POINTI TATU ZA MASHUJAA

SELEMAN Matola, kocha msaidizi wa Simba SC amesema kuwa wanatambua mpinzani wao Mashujaa FC yupo imara wataingia kucheza kama fainali ili kufikia malengo yakupata pointi tatu.

Ni mchezo wa mzunguko wa pili kati ya Simba SC dhidi ya Mashujaa FC unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC Complex ikiwa ni mzunguko wa pili.

Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, Novemba Mosi 2024 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Mashujaa FC 0-1 Simba SC bao la ushindi likifungwa na Steven Mukwala dakika ya 90 akitumia pasi ya Awesu Awesu.

Nyota hao wote wa Simba SC ambao walihusika kwenye bao la ushindi mchezo uliopita wote walianzia benchi na walipoingia walitimiza majukumu waliyopewa kwenye msako wa pointi tatu muhimu.

Matola amesema: “Tunatambua mchezo wetu utakuwa mgumu kwa kuwa wapinzani wetu wapo imara ila tutaingia kwa umakini na kucheza kama fainali kufikia malengo yetu ya kupata pointi tatu muhimu.”

Simba SC kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya pili na pointi 57 inakutana na Mashujaa FC ambao kwenye msimamo wapo nafasi ya 10 na pointi 30.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.