MFUNGAJI BORA MUUNGANO CUP HUYU HAPA

MAXI Nzengeli ni mfungaji bora Muungano Cup 2025 akifunga jumla ya mabao mawili kwenye mechi tatu ambazo Yanga SC imecheza.

Nzengeli alifungua ukurasa wa mabao katika mchezo wa hatua ya nusu fainali dhidi ya Zimamoto ilikuwa Aprili 29 2025 alipopachika bao dakika ya 29.

Kwenye mchezo huo baada ya dakika 90 ubao wa Gombani ulisoma Zimamoto 1-1 Yanga SC, bao la Zimamoto lilifungwa na Saidi Mwinyi dakika ya 71.

Yanga SC ilitinga hatua ya fainali kwa ushindi wa penati ambapo ilikuwa Zimamoto 1-3 Yanga SC, langoni kwa Yanga SC alianza Aboutwalib Mshery.

Bao la pili Nzengeli alipachika kwenye mchezo wa fainali dhidi ya JKU SC ilikuwa ni Mei Mosi 2025.

Baada ya dakika 90 ubao ukasoma JKU SC 0-1 Yanga SC, bao la ushindi lilipachikwa dakika ya 45 na likadumu mpaka mwisho wa mchezo huo.

Yanga SC ni mabingwa wa Muungano Cup 2025, hatua ya robo fainali Yanga SC ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KVZ FC, mabao ya Aziz Ki dakika ya 29 na Dennis Nkane dakika ya 85.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.