MASHUJAA FC SIO KINYONGE KUIKABILI SIMBA SC

BENCHI la ufundi la Mashujaa FC limebainisha kuwa limefanya maandalizi mazuri kuelekea mchezo wa mzunguko wa pili dhidi ya Simba SC unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC Complex saa 10:00 jioni.

Ipo wazi kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Lake Tanganyika baada ya dakika 90 ubao ulisoma Mashujaa 0-1 Simba, Steven Mukwala alipachika bao la ushindi akiwa ndani ya 18 dakika ya 90.

Kocha msaidizi wa Mashujaa FC, Charles Fredie amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu kwa kila timu kupambana kupata pointi tatu muhimu nao wamefanya maandalizi mazuri kuwakabili wapinzani wao.

“Mchezo  dhidi ya Simba SC tumejiandaa kufanya vizuri kuliko mchezo wa awali waliopata ushindi dakika za mwisho. Changamoto itakuwa kubwa sana kwani tunafahamu tunaenda kukutana na timu nzuri lakini tumejiandaa kukabiliana nao.

“Kuanzia kwenye eneo la ushambuliaji na ulinzi wachezaji wapo imara hivyo tutakabiliana na wapinzani wetu kwa namna ambavyo watakuja kwenye mchezo wetu.”

Mashujaa FC kwenye msimamo nafasi ya 10 baada ya mechi 26 ni pointi 30 kibindoni imekusanya msimu wa 2024/25. Inakutana na Simba SC iliyo nafasi ya pili kwenye msimamo pointi 57 baada ya mechi 22.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.