YANGA SC KUSHUSHA FULL MUZIKI FAINALI MUUNGANO CUP

YANGA SC inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi Mei Mosi 2025 inatarajiwa kuwa na kibarua kwenye mchezo wa fainali Muungano Cup dhidi ya JKU SC Uwanja wa Gombani, Pemba.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa saa 1:15 usiku ambapo Yanga SC imebainisha kuwa itaongeza uzito kwenye mchezo huo hasa katika eneo la wachezaji ambapo huenda wakashusha full muziki kwa ajili ya kuwakabili wapinzani wao.

Katika mechi ya robo fainali na nusu fainali kuna wachezaji wa Yanga ambao walikuwa wakianzia benchi miongoni mwao ni Dickson Job ambaye ni nahodha, Djigui Diarra ambaye ni kipa namba moja wa Yanga na katika mchezo wa nusu fainali ni Aboutwalib Mshery alianza kikosi cha kwanza.

Ali Kamwe,  Ofisa Habari wa Yanga ameweka wazi kuwa kuelekea mchezo wa fainali wataongeza uzito ili kupambania taji hilo dhidi ya wapinzani wao ambao wapo imara kwenye mechi ambazo wamecheza.

Ikumbukwe kwamba JKU SC ilianza kuwaondoa Singida Black Stars kwenye hatua ya robo fainali kisha Azam FC kwenye hatua ya nusu fainali huku Yanga iliwandoa KVZ kwenye robo fainali na Zimamoto kwenye hatua ya nusu fainali.

Zimamoto iliwafungashia virago Coastal Union ya Tanga hivyo timu tatu zinazoshiriki Ligi Kuu Tanzania Bara ziliondolewa mapema katika Muungano Cup.

“Tutawaongezea uzito kidogo wapinzani wetu JKU kwenye fainali huu ni mchezo muhimu kwetu na tunatambua kwamba mabingwa wanakutana.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.