NDANI ya Ligi Kuu Bara, Simba ni namba moja katika timu zilizofunga mabao mengi ya penalti ambazo ni 10 kwa msimu wa 2024/25.
Kwenye penalti hizo ni 9 zilifungwa huku moja ilikoswa na Leonel Ateba ilikuwa dhidi ya Namungo FC Uwanja wa Majaliwa. Katika mchezo huo Simba SC ilipata penati tatu, mbili zilifungwa na Jean Ahoua huku moja ikikoswa na Ateba baada ya Jonathan Nahimana kuokoa penati hiyo.
Jean Ahoua katupia mabao 12 na katika mabao hayo ni mabao matano kafunga kwa penalti, katika penalti tano ambazo alipewa apige Ahoua zote alifunga msimu wa 2024/25.
Simba SC Mei 2 2025 itakuwa na kazi kwenye msako wa pointi tatu dhidi Mashujaa FC unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC Complex ikiwa ni mzunguko wa pili katika mchezo wa mzunguko wa kwanza Simba SC ilipata pointi tatu kwa ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Steven Mukwala.
Singida Black Stars ni namba mbili kupata penalti nyingi ambazo ni 8, Mashujaa FC, Yanga na Namungo FC hizi zimepata penalti 7.
Kwa Yanga penati nne zilifungwa na Aziz Ki akikosa penati mbili na moja ilifungwa na Pacome dhidi ya Kagera Sugar.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.