Klabu ya RS Berkane ya Morocco imeifuata Simba Sc kwenye fainali ya kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) kufuatia ushindi wa jumla wa 4-1 dhidi CS Constantine ya Algeria kwenye nusu fainali licha ya kupoteza 1-0 kwenye mchezo wa mkondo wa pili.
FT: CS Constantine 🇩🇿 1-0 🇲🇦 RS Berkane (Agg. 1-4)
⚽ 47’ Belhocini
RS Berkane ambayo ilishinda 4-0 kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza itacheza fainali na Simba Sc ya Tanzania ikianzia nyumbani kwenye fainali ya kwanza Mei 17, 2025 katika dimba la Manispaa ya Berkane huko Morocco.
Timu hizo zitarudiana Mei 25, 2025 hapa Tanzania ingawa bado haijabainika ni wapi mchezo huo utapigwa kati ya New Amaan Complex, Zanzibar au Benjamin Mkapa kulingana na mwenendo wa maboresho yanayoendelea kwenye dimba la Mkapa.