MATAJIRI wa Dar, Azam FC leo Aprili 28 2025 wanatarajiwa kuwa kazini kwenye mchezo wa nusu fainali Muungano Cup, visiwani Zanzibar katika dakika 90 za kazi kusaka tiketi yakutinga hatua ya fainali.
Azam FC itakuwa Uwanja wa Gombani, Pemba, leo Jumatatu saa 1.15 usiku kuvaana na JKU ambayo iliwafungashia virago Singida Black Stars hatua ya robo fainali huu utwakuwa ni mchezo wa nusu fainali.
Mshindi wa mchezo wa leo anatarajiwa kukutana na mshindi wa mchezo wa Aprili 29 2025 ambao utawakutanisha Zimamoto iliyowaondoa Coastal Union ya Tanga kwa bao 1-0 dhidi ya Yanga SC iliyowapenya nusu fainali kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya KVZ.
Mabao ya Yanga yalifungwa na Aziz Ki na Dennis Nkane ambaye alianzia benchi alifunga bao kwenye mchezo huo dakika ya 86.
Aprili 25 2025 Azam FC ilitinga nusu fainali kwa ushindi mbele ya KMKM 0-1 Azam FC bao likifungwa na Lusajo Mwaikenda na kiungo James Akamiko alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.