AHOUA ALIYEKOSA NAFASI YA DHAHABU KIMATAIFA YUPO KAMILI

KIUNGO mshambuliaji wa Simba Ahoua kwenye mchezo dhidi ya Stellenbosch FC alipata maumivu ya nyama za misuli dakika ya 86 alirejea uwanjani kukamilisha dakika nne zilizobaki.

Kwenye mchezo huo akiwa ndani ya 18 na mpira alikosa nafasi ya wazi dakika ya 90 kwa shuti lake kwenda nje ya lango baada yakupewa pasi kutoka kwa nyota Ellie Mpanzu.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba ameweka wazi kuwa kwa sasa kiungo huyo anaendelea vizuri baada ya kupata matibabu jambo ambalo limefanya awe sehemu ya kikosi kilichopo Afrika Kusini.

“Jean Ahoua kwa sasa anaendelea vizuri na yupo tayari kwa mchezo ujao kwani alipata maumivu ya nyama za misuli kisha akarudi uwanjani na alipewa matibabu yupo tayari kuwapa burudani Wanasimba.

“Tupo kwenye mapambano makubwa ambapo tunahitaji kuona timu inatinga hatua ya fainali hilo linawezekana kutokana na ubora wa wachezaji tulionao na benchi la ufundi makini.”.

Aprili 27 2025 ni Stellenbosch FC vs Simba SC nchini Afrika Kusini, mshindi wa mwisho atatinga hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.