SIMBA YAKWEA PIPA KUELEKEA AFRIKA KUSINI

KIKOSI cha Simba chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids mapema Aprili 23 2025 kimekwea pipa kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Stellenbosch FC unaotarajiwa kuchezwa Aprili 27 2025.

Ipo wazi kwamba kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Amaan, baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 1-0 Stellenbosch FC hivyo mchezo wao wa pili unakwenda kukamilisha msindi atakayekwenda kucheza hatua ya fainali.

Bao la Simba kwenye mchezo huo lilifungwa na nyota Jean Ahoua dakika ya 44 kwa pigo huru ambalo kulingana na namna wachezaji wa Simba walivyokuwa karibu na eneo la lango mwamuzi alikwenda kujiridhisha kwenye VAR hatimaye bao likakubalika.

Miongoni mwa wachezaji waliopo kwenye msafara ni Jean Ahoua, Moussa Camara, Kibu Dennis, Zimbwe, Shomari Kapombe, Kagoma Yusuph,Che Malone, Ally Salim.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wanakwenda kupambana kwa ajili yakwenda hatua ya fainali Kombe la Shirikisho Afrika.

“Tunakwenda kupambana kwa ajili yakusaka ushindi na malengo yetu nikuona kwamba tunakwenda fainali. Ninawaambia ndugu zangu Waandishi wa Habari nendeni mkawaambie Watanzania kwamba Simba anakwenda fainali.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.