Klabu ya Simba Sc imekuwa kinara kwenye orodha ya timu zinazofanya vizuri kwa wiki ya 21 iliyotolewa na mtandao wa Africa Soccer Zone Power huku miamba wengine wa Tanzania, Yanga Sc wakikamata nafasi ya nne.
Mabingwa wapya wa Morocco, RS Berkane wapo nafasi ha pili, vigogo wa Misri, Pyramids wanakamata nafasi ya tatu huku Mabingwa wa Afrika, Al Ahly wakikamilisha tano bora.
Orlando Pirates (6), Power Dynamos(7), Esperance Tunis(8), Mamelodi Sundowns(9) na Vipers Sc(10) wanakamilisha 10 bora.