MKALI wa mabao ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Clement Mzize amefichua kilicho nyuma ya mafanikio yake kwenye kusepa na tuzo.
Mzize kwenye mchezo dhidi ya Fountain Gate uliochezwa Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa Aprili 21 aliibuka kuwa mchezaji bora ubao uliposoma Fountain Gate 0-4 Yanga.
Ushindi huo unaifanya Yanga iifunge mabao 9 mbele ya Fountain Gate ndani ya dakika 180 kwa kuwa kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza ilikuwa Yanga 5-0 Fountain Gate hivyo kwenye msako wa pointi sita, Yanga wamekomba zote huku Fountain Gate wakiyeyusha pointi sita mazima.
Mzize ameweka wazi kuwa ni tuzo yake ya tatu kutwaa ndani ya ligi namba nne kwa ubora Afrika kwenye mechi za ushindani uwanjani msimu wa 2024/25.
“Hii ni tuzo yangu ya tatu kwenye mechi za ligi, yote hii inatokana na juhudi kwenye mechi zote ambazo tunacheza, ushirikiano na wachezaji, benchi la ufundi malengo yetu nikuona kwamba tunapata ushindi katika mechi zote uwanjani.
“Mazoezi ninayofanya nayo ni sehemu ya sababu yakuwa kwenye ubora kwa kuwa mpira ni kazi basi tunaifanya kwa kujituma.”
Mzize ni namba moja wa wakali wakucheka na nyavu akiwa anaongoza chati hiyo baada yakufikisha mabao 13 ndani ya ligi.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.