Klabu ya Simba Sc imetangaza kuwa kikosi cha wachezaji 23 cha timu hiyo kitaondoka kesho asubuhi kuelekea Afrika Kusini kwa ajili ya mchezo wa mkondo wa pili wa hatua ya nusu fainali ya kombe la Shirikisho Afrika (CAFCC) dhidi ya Stellenbosch.
Kikosi hicho kitaondoka na Ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) ikipitia Johannesburg kabla ya kuunganisha kuelekea Durban ambapo mahali ambapo mchezo huo utapigwa siku ya Jumapili, Aprili 27, 2027.
Simba Sc wanaelekea Sauzi wakiwa na mtaji wa goli moja kwa ‘nunge’ kufuatia ushindi wa 1-0 dhidi ya Stellenbosch kupitia kwa goli la mshambuliaji Jean Charles Ahoua kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza wa CAFCC katika dimba la New Amaan Complex, Zanzibar.