Kocha wa Timu ya soka ya Taifa ya Kenya ‘Harambee Stars’ Benni McCarthy amepigiwa upatu kuwa Kocha wa Klabu yake ya zamani.
Kocha wa Harambee Stars ameibuka miongoni mwa majina yanayohusishwa na nafasi ya Ukocha katika miamba ya Afrika Kusini Orlando Pirates.
Gwiji huyo wa Bafana Bafana amehudumu miezi michache tu tangu ateuliwe kuwa Kocha Mkuu wa Harambee Stars, baada ya kuchukua wadhifa huo Machi 3.
Mkufunzi huyo wa Harambee Stars amehusishwa na jukumu la kuinoa miamba hiyo ya Afrika Kusini kufuatia ripoti kwamba kocha wa Orlando Pirates, Jose Riveiro anatarajiwa kuondoka katika klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.