BEKI wa Yanga, Israel Mwenda amesema kuwa ambacho wanahitaji kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Fountain Gate, Aprili 21 ni pointi tatu muhimu baada ya dakika 90.
Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza, Yanga ilipata ushindi wa mabao 5-0 mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex.
Mwenda ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Miloud Hamdi ameweka wazi kuwa wanahitaji ushindi kwenye mchezo huo kutokana na umuhimu wa pointi tatu ndani ya uwanja.
“Tunahitaji pointi tatu muhimu kwenye mchezo wetu dhidi ya Fountain Gate ambao utakuwa ni mchezo mgumu na wenye ushindani hilo tunalitambua.
“Wachezaji tupo tayari kwa ajili yakupata matokeo chanya hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani kwa ajili ya kushuhudia mchezo wetu watashangilie.”
Mbali na Mwenda wachezaji waliopo Manyara kwa ajili ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ni Maxi Nzengeli, Dickson Job, Mudathir Yahya.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.