HIKI hapa kikosi cha Simba kitakachoanza mchezo dhidi ya Stellenbosch FC ya Afrika Kusini mchezo wa hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika ikiwa ni nusu fainali ya kwanza.
Kikosi cha kwanza langoni yupo Moussa Camara, wengine eneo la ulinzi ni Chamou, Hamza Jr, Mohamed Hussen, Shomari Kapombe, kwa viungo ni Fabrice Ngoma.
Jean Ahoua, Steven Mukwala, Ellie Mpanzu na Kibu Dennis hawa wamekuwa wakitumika kwenye eneo la ushambuliaji na Yusuph Kagoma katika eneo la ukabaji.
Akiba ni Ally Salim, Duchu, Nouma, Edwin Balua, Okejepha, Mavambo, Awesu, Mutale, Leonel Ateba. Uwanja wa New Amaan.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.