MCHAMBUZI wa soka Bongo, Mbwaduke amebainisha kuwa Klabu ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids inatengeneza nafasi nyingi kwenye mechi zake za ushindani tatizo lipo kwenye umaliziaji kubadili nafasi hizo kuwa bao ndani ya uwanja. Safu ya ushambuliaji ya Simba inaongozwa na Leonel Ateba ambaye amefunga mabao 8 katika hayo manne ni kwa penati na katika penati 5 ambazo alipewa jukumu la kupiga alikosa penati moja dhidi ya Namungo.