NYOTA wa kikosi cha Azam FC, Pascal Msindo beki wakupanda na kushuka bado hajawa imara kwa sasa kutokana na maumivu ambayo aliyapata kwenye mchezo wa ushindani ndani ya ligi namba nne kwa ubora Afrika.
Ilikuwa ni mbele ya Yanga katika mchezo wa Dar Dabi beki huyo alipata maumivu baada ya kuchezewa faulo na beki Kibwana Shomari.
Kwenye mchezo huo Azam FC ilipoteza Dar Dabi kwa ubao wa Uwanja wa Azam Complex kusoma Azam FC 1-2 Yanga pointi tatu zikiwa ni mali ya Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi.
Ni Pacome alipachika bao la utangulizi kwa Yanga dakika ya 11 na Prince Dube alipachika bao la pili dakika ya 33 kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa.
Pacome alikwama kukamilisha dakika 90 pia kwenye mchezo huo baada ya kupata maumivu hivyo nafasi yake ilichukuliwa na Clement Mzize ambaye ni mshambuliaji.
Bao la Azam FC kwenye mchezo huo lilifungwa na Lusajo Mwaikenda dakika ya 86 kipindi cha pili akimtungua mlinda mlango Diarra ambaye alianza kikosi cha kwanza na upande wa Azam FC ni Zuber Foba alianza langoni.
Azam FC kwenye msimamo wa ligi ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 51 baada yakucheza mechi 26, vinara wa ligi ni Yanga wenye pointi 67 baada yakucheza mechi 25.
Get well soon Msindo…
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.