ZIDANE Sereri nyota wa Azam FC ameweka wazi kuwa kuna dhana ya kukatishana tamaa kwenye masuala ya upambanaji jambo ambalo linasababisha wengi kukwama kufikia malengo yao.
Nyota huyo atakumbukwa na kipa Moussa Camara wa Simba kwenye Mzizima Dabi alimtungua bao la jioni akiwa ndani ya 18 mwisho ubao ukasoma Simba 2-2 Azam FC na alichaguliwa kuwa mchezaji bora kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa.
Sereri amesema: “Watu wananiambia mimi sijafikia muda sahihi kwa sasa kufanya kazi kubwa lakini mimi huwa ninawauliza muda wangu sahihi ni upi? Labda nikifika miaka 30 ama 40? Hapo wanashindwa kunipa ukweli.
“Kuhusu kucheza hakuna suala la kuhofia kukaa benchi, hivyo suala la kucheza ni jitihada za mchezaji mwenyewe haijalishi kwamba wewe una kiwango ama hauna kiwango kikubwa ni jitihada.
“Ambacho kinatakiwa kwa sasa ni kufanya vizuri na kupewa nafasi kwenye mechi ambazo tunapata, na muda ambao upo sio kuhofia kukaa benchi hakuna mchezaji ambaye hajawahi kukaa benchi hata wale wakubwa unaonawa walikaa benchi.
“Vijana wadogo kwa sasa ni mud awa kujitoa na kufanya kweli kwenye mechi na kupambania ndoto kwa kuwa kila mahali kuna ushindani n ahata Azam FC kuna ushindani lakini tunahitaji kufanya vizuri kila mchezo.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.