KIUNGO wa Yanga, Pacome amepachika bao pekee la ushindi kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Coastal Union uliochezwa Uwanja wa KMC Complex dakika ya 34 kipindi cha kwanza akitumia pasi ya Maxi Nzengeli.
Pacome amekuwa kwenye ubora wake na katika mchezo dhidi ya Tabora United, Aprili 2 2025 alitoa pasi mbili za mabao alimpa Prince Dube na Clement Mzize ambao hawa wote wamefikisha mabao 11 ndani ya ligi.
Coastal Union msimu wa 2024/25 mbele ya Yanga imepoteza nje ndani, mchezo wa kwanza ilikuwa Coastal Union 0-1 Yanga na mchezo wa mzunguko wa pili Coastal Union imepoteza kwa mara nyingine tena hivyo Yanga imekomba pointi zote sita kwa Wagosi Wakaya.
Clatous Chama aliingia kipindi cha pili dakika ya 83 akichukua nafasi ya Maxi Nzengeli, Kenned Musonda naye aliingia dakika ya 83 akichukua nafasi ya Prince Dube.
Nyota mwingne ambaye alipata maumivu kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union ni Nickson Kibabage dakika ya 82 nafasi yake ilichukuliwa na Kibwana Shomari dakika ya 83.
Nyota Khalid Aucho alikwama kukomba dakika 90 baada yakupata maumivu dakika ya 45 kipindi cha kwanza jambo ambalo lilimfanya atoke nje ya uwanja akionekana kuwa na masikitiko makubwa.
Nafasi yake ni kiungo Mudathir Yahya aliingia kipindi cha pili kuendelea pale ambapo kiungo huyo wa kazi mwili jumba aligotea kwenye dakika 45 za mwanzo.
Dakika ya 69 kipa wa Coastal Union, Fales Gama alipata maumivu baada ya kugongana na beki Lameck Lawi kweye harakati za kuokoa mpira ndani ya 18 walipokuwa wakipambania kuweka lango salama.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.