UONGOZI wa Simba umebainisha kuwa haupo tayari kugotea kwa mara nyingine tena kwenye hatua ya robo fainali kwenye mashindano ya kimataifa Afrika malengo ni kuona wanavuka hatua hiyo na kutinga hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika.
Katika mchezo wa kwanza wa robo fainali wakiwa ugenini nchini Misri, Aprili 2 2025 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Suez Canal ulisoma Al Masry 2-0 Simba, kibarua cha mwisho inatarajiwa kuwa Aprili 9 2025 Uwanja wa Mkapa kwenye hatua ya robo fainali ya pili.
Mchezo wa hatua ya pili unatarajiwa kukamilisha dakika 180 ambazo zitatoa mshindi wa jumla kwenye mchezo huo atakayesonga mbele hatua ya nusu fainali Kombe la Shirikisho Afrika.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa inatosha kwa maumivu ambayo walipitia kushindwa kutinga hatua ya robo fainali kwenye mechi zilizopita watapambana kupata matokeo mazuri.
“Kwenye mechi zetu zilizopita hatua yar obo fainali tulipata maumivu, tuliishia hapa mara nyingi hatutaki hili litokee tena, unyonge katika hatua hii basi kwa kuwa tupo tayari na tuna kikosi chenye wachezaji wapambanaji kwelikweli.
“Makosa yaliyotokea ugenini tunasahau na benchi la ufundi linayafanyia kazi ili kuwa imara kwa mchezo wetu ujao, hakuna sababu kuanza kumpa mtu lawama wakati huu hili ni letu sote na tuungane kushirikiana ili kupata matokeo mazuri.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.