BAADA ya kumalizana na Tabora United katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi kituo kinachofuata kwa Yanga ni Coastal Union.
Aprili 2 2025 ubao ulisoma Tabora United 0-3 Yanga, mabao ya Israel Mwenda kwa pigo la faulo, Clement Mzize na Prince Dube yaligota mpaka mwisho wa dakika 90.
Yanga ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 61 na safu ya ushambuliaji imefunga mabao 61 ikiwa ni timu namba moja kwa kufunga mabao mengi msimu wa 2024/25.
Mchezo ujao ni dhidi ya Coastal Union unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC Complex, Aprili 7 2025 saa 10:00 jioni.
Walter Harrison, Meneja wa Yanga ameweka wazi kuwa mpango mkubwa kwenye mechi ambazo wanacheza ni kupata pointi tatu muhimu.
“Kwenye mechi zetu zote ambacho tunahitaji ni pointi tatu muhimu, tunajua kuna ushindani lakini tupo tayari.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.