WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye anga la kimataifa Simba wakiwa wapo hatua ya robo fainali wamebainisha kuwa kugotea mara nyingi hatua ya robo fainali kumewapa somo kubwa ambalo hawataki kuona linajirudia tena kwa msimu wa 2024/25.
Kwenye mchezo wa kwanza wa robo fainali wakiwa ugenini, Simba walishuhudia ubao wa Uwanja wa Suez Canal ukisoma Al Masry 2-0 Simba kibarua kipo Aprili 9 kwa Simba kupambana na Waarabu wa Misri kusaka ushindi kukata tiketi ya hatua ya robo fainali wakipindua meza, ikiwa matokeo hayatabadilika safari yao itakuwa imefika tamati.