KWENYE kasi ya kuwania kiatu cha ufungaji bora kuna vita mpya msimu wa 2024/25 kukiwa na balaa zito kutokana na kila mchezaji kuwa na nyota kweye kucheka na nyavu ndani ya ligi kuu bara ambayo ni namba nne kwa ubora.
Ipo wazi msimu wa 2023/24 ni Aziz Ki wa Yanga alikuwa mfungaji bora na mabao yake 21, msimu huu katupia mabao 7 sawa na idadi ya pasi zake za mabao.
Clement Mzize nyota anayetimiza majukumu yake ndani ya kikosi cha Yanga huyu ni mzawa pekee mwenye mabao mengi ndani ya chati ya wafungaji bora akiwa katupia mabao 11 kibindoni sawa na Prince Dube raia wa Zimbabwe.
Jean Ahoua kiungo wa Simba ana mabao 12 yeye ni raia wa Ivory Coast. Hivyo kwenye chati ya utupiaji wageni wamekuwa na zali lakucheka na nyavu zaidi.
Steven Mukwala raia wa Uganda ni mali ya Simba huyu ni mabao 9 katupia, Elvis Rupia raia wa Kenya yupo Singida Black Stars mabao 9, Gibrill Sillah wa Azam FC huyu ni Mgambia, Jonathan Sowa mali ya Singida Black Stars ni Mghana, Peter Lwasa raia wa Uganda yupo Kagera Sugar na Leonel Ateba wa Simba raia wa Cameroon hawa wote wana mabao 8.
Ligi namba nne kwa ubora Afrka kwa sasa ni mzunguko wa pili kila timu inapambana kutimiza malengo yake na msako ni mkali kwa timu ambazo zinapambania kutwaa ubingwa na zile ambazo zinapambania kutoshuka daraja.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.