YANGA YATUMA UJUMBE HUU TABORA UNITED

UONGOZI wa Yanga umebainisha kuwa unazitaka pointi tatu za Tabora United kwenye mchezo wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi hivyo wataingia kwa tahadhari kuwakabili wapinzani wao.

Novemba 7 2024 baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Azam Complex ulisoma Yanga 1-3 Tabora United, pointi tatu ziliyeyuka mazima kwa mabingwa watetezi wa ligi zama za Miguel Gamondi.

Kamwe amesema kuwa wanatambua mchezo huo utakuwa ni mgumu na wenye ushindani mkubwa lakini maandalizi yaliyofanyika yanawapa imani kupata pointi tatu muhimu uwanjani.

“Hautakuwa mchezo rahisi kwani wapinzani wetu nao wanahitaji matokeo, kwetu ni muhimu kupambana kwa wachezaji kujitoa na kujituma kwenye mazoezi ya mwisho tumeona namna hali ilivyokuwa tuna imani kupata pointi tatu muhimu.”

Tabora United kwa sasa ipo chini ya Genesis Mang’ombe huyu ni kocha anatarajiwa kukaa benchi Aprili 2 2025 baada ya kuchukua mikoba ya Anicet Kiazmak aliyekuwa benchi kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza wakati Yanga ikipoteza pointi tatu mazima.

Kwenye msimamo Tabora United ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 37 baada ya mechi 23, ushindi ni kwenye mechi 10. Ilipoteza mechi 6 ikiambulia sare kwenye mechi 7 ndani ya msimu wa 2024/25 na safu ya ushambuliaji imetupia mabao 27 ukuta umeruhusu mabao 28.

Tabora United inakutana na safu namba moja kwa kufunga mabao mengi ndani ya ligi ambayo ni 58 na Yanga ni vinara kwenye ligi wakiwa na pointi 58 pia.

 

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.