KIKOSI CHA SIMBA DHIDI YA AL MASRY, CAMARA NDANI

MOUSSA Camara kipa namba moja wa Simba amepangwa kuanza kikosi cha kwanza dhidi ya Al Masry mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Suez, saa 1:oo kwa saa za Afrika Mashariki.

Simba inakibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Al Masry mchezo wa hatua ya robo fainali ambapo mbali na Camara ni Chamou, Fabrince Ngoma, Jean Ahoua, Shomari Kapombe, Leonel Ateba, Hamza Jr, Mohamed Hussen, Yusuph Kagoma, Ellie Mpanzu na Kibu Dennis wameanza.

Wachezaji wa akiba ni Ally Salim, Duchu, Nouma, Okejapha, Ladack Chasambi, Mavambo, Awesu, Joshua Mutale na Steven Mukwala.

Mchezo wa robo fainali ya pili unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa itakuwa ni Aprili 9 2025, mshindi wa jumla atatinga hatua ya nusu fainali.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.