OFISA Habari wa Fountain Gate, Issa Liponda maarufu kwa jina la Mbuzi amesema kuwa hakuna namna yoyote anayoona kwa wapinzani wao Singida Black Stars wakitoka kwenye mchezo wao wa ligi unaotarajiwa kuchezwa Aprili 2 2025.
Ni Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa, Manyara mchezo huo unatarajiwa kuchezwa saa 10:15 kwa wababe hawa wawili kusaka pointi tatu muhimu ndani ya uwanja.
Kwenye msimamo Fountain Gate ni nafasi ya 7 ikiwa na pointi 28 baada ya kucheza mechi 23 inakutana na Singida Black Stars ambayo ipo nafasi ya nne na pointi 44 baada yakucheza mechi 23.
Ndani ya dakika 2,070 Fountain Gate ilipata ushindi kwenye mechi 8, ilipata sare kwenye mechi nne ikipoteza mechi 11, safu ya ushambuliaji imetupia mabao 28 na ukuta umeruhusu mabao 40 inakutana na Singida Black Stars ambayo safu ya ushambuliaji imetupia mabao 32 na ukuta ukiruhusu kufungwa mabao 19.
Fountain Gate haijawa imara kwenye eneo la ulinzi ambapo inaingia kwenye orodha ya timu ambazo zimefungwa mabao mengi zaidi ndani ya ligi ikiwa na wastani wakufungwa bao moja kila baada ya dakika 51 inakutana na timu ambayo ina wastani wakufungwa bao moja kila baada ya dakika 108.
Mbuzi amesema: “Hakuna namna kwa mchezo wetu tukiwa nyumbani lazima pacha apigwe chuma kama mbili ama tatu kwa kuwa maandalizi ambayo yamefanyika na benchi la ufundi sioni nafasi kwa Singida Black Stars kutoka safari hii kwenye mchezo wetu, mashabiki mjitokeze kwa wingi kushuhudia burudani.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.