MILOUD Hamdi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema watapambana kufanya kazi kubwa mbele ya Tabora United ili wapate pointi tatu muhimu katika mchezo ujao unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya dakika 90.
Machi 2025 Yanga ilifunga kwa kupata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Songea United mchezo wa CRDB Federation Cup ilikuwa ni Machi 29 ambapo mabao yalifungwa na Duke Abuya dakika ya 22 na Jonathan Ikanga Lombo dakika ya 54.
Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex nyota wa Yanga Pacome Zouzoua alichaguliwa kuwa mchezaji bora na kupewa zawadi ya laki tano na mdhamini benki ya CRDB.
Miloud amesema wachezaji wanajituma kwenye kutafuta ushindi jambo ambalo linawapa nguvu kushinda na kila mchezo wanautazama kwa umuhimu ndani ya uwanja.
“Kila mchezo ambao tunacheza kwetu tunauchukulia kwa umuhimu ambacho tunahitaji ni kupata pointi tatu, mashabiki wazidi kuwa nasi kwani tunatambua mchezo ujao utakuwa ni wa ligi na ushindani ni mkubwa.”
Mchezo ujao kwa Yanga kwenye ligi ni dhidi ya Tabora United unatarajiwa kuchezwa Aprili 2 2025 kwa vinara hao wenye pointi 58 kushuka uwanjani.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.