MTAMBO WA MABAO YANGA KAMILI KWA KAZI

MTAMBO wa mabao ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi upo kamili kwa mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Aprili 2 2025, Tabora.

Ni Prince Dube chaguo la kwanza la kocha ni miongoni mwa wachezaji ambao wapo kwenye kikosi cha Yanga ambacho kinakumbuka kwamba mzunguko wa kwanza walipoteza pointi tatu mazima Uwanja wa Azam Complex uliposoma Yanga 1-3 Tabora United.

Dube kahusika kwenye mabao 17 kati ya 58 yaliyofungwa na Yanga ambapo katika mabao hayo 6 kafunga kwa kichwa matatu kafunga kwa mguu wa kulia na moja akitumia mguu wa kushoto ni namba moja kwa mastaa wenye mabao mengi ya vichwa.

Ni mabao 10 anayo kibindoni na pasi 7 za mabao alizotengeneza msimu wa 2024/25 na Yanga inaongoza kuwa na mabao mengi kibindoni ambayo ni 58 sawa na pointi zao wakiwa nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi.

Ni mechi 20 amecheza ndani ya ligi akikomba dakika 1,354 anashikilia rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kufunga hat trick ndani ya ligi ambapo aliwatungua Mashujaa Desemba 19 2024.

Tayari kikosi cha Yanga kimewasili salama Tabora kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.