TABORA United itawakabili mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika, Yanga bila uwepo wa mchora ramani ya ushindi kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza walipokutana katika dakika 90 zakuvuja jasho.
Mpaka mchora ramani huyo anakutana na Thank You rekodi zinaonyesha kuwa alikaa benchi kwenye jumla ya mechi 14, ushindi mechi 8 sare ilikuwa katika mechi 5 na alipoteza mchezo mmoja ndani ya msimu wa 2024/25 Anicet Kiazmak.
Ndani ya dakika 1,260 alizokaa benchi ushindi ilikuwa ni dakika 720, sare dakika 450 na kupoteza dakika 90 anaingia kwenye orodha ya timu zilizopata ushindi mkubwa mbele ya Yanga kwa msimu wa 2024/25 ndani ya uwanja ugenini.
Kwenye msimamo Tabora United ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 37 baada ya mechi 23, ushindi ni kwenye mechi 10 katika hizo moja ilivuna pointi tatu mazima ugenini dhidi ya Yanga ambao ni mabingwa watetezi.
Ilipoteza mechi 6 ikiambulia sare kwenye mechi 7 ndani ya msimu wa 2024/25 na safu ya ushambuliaji imetupia mabao 27 ukuta umeruhusu mabao 28.
Christina Mwagala, Ofisa Habari wa Tabora United ameweka wazi kuwa wanatambua wapinzani wao wanahitaji kulipa kisasi cha kupoteza mchezo uliopita hilo wasahau kwa kuwa wapo imara na wanhitaji pointi tatu.
“Tutakuwa nyumbani kwenye mchezo wetu ujao kikubwa tunahitaji pointi tatu kwa kuwa kazi yetu ni kuleta ushindani, tulipata ushindi mzunguko wa kwanza na sasa tunahitaji alama nyingine mbele yao, mashabiki wawe pamoja nasi kwani hili linawezekana.”
Ikumbukwe kwamba katika mchezo wa mzunguko wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Azam Complex baada ya dakika 90, Novemba 7 2024 ubao ulisoma Yanga 1-3 Tabora United, bao la kufutia machozi kwa Yanga lilifungwa na Clement Mzize.
Kocha aliyekuwa benchi kwenye mchezo huo kwa sasa hayupo kwani timu ipo chini ya Genesis Mang’ombe huyu ni kocha anatarajiwa kukaa benchi Aprili 2 2025 baada ya kuchukua mikoba ya Anicet Kiazmak aliyekuwa benchi kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.