AZAM FC YAIPIGIA HESABU GEITA GOLD

MATAJIRI wa Dar, Azam FC wanapiga hesabu kuvuna pointi tatu ugenini dhidi ya Ken Gold mchezo unaotarajiwa kuchezwa Aprili 3 2025 Uwanja wa Sokoine ikiwa ni mzunguko wa pili.

Baada ya mechi 23 ambazo ni dakika 2,070 Azam FC imekusanya jumla ya pointi 48 ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo, safu ya ushambuliaji imetupia mabao 36 huku nyota aliyehusika kwenye mabao mengi akiwa ni kiungo mshambuliaji Feisal Salum mwenye mabao manne na pasi 12 akihusika katika jumla ya mabao 16.

Ikumbukwe kwamba Feisal ni namba moja kwa wachezaji wenye pasi nyingi za mabao za mwisho akiwa nazo 12 kwa msimu wa 2024/25 akivunja rekodi yake ya msimu wa 2023/24 alipotoa pasi 7 za mabao.

Thabit Zakaria, Mkuu wa Idara ya Habari Azam FC ameweka wazi kuwa wanatambua ushindani ni mkubwa na hesabu ni kupata pointi tatu kwenye mechi ambazo watacheza ndani ya uwanja.

“Kwenye kufukuzia malengo ni muhimu kupata pointi tatu kwa kuwa kila timu ambayo tunacheza nayo haina muda wakupoteza nayo inahitaji pointi tatu vilevile, mechi zina ushindani mkubwa nasi tupo tayari kwa ajili ya mechi zetu zote, mashabiki wawe pamoja nasi.”

Ken Gold kwenye msimamo ipo nafasi ya 16 ikiwa imekusanya pointi 16 baada ya kucheza mechi 23 ina wastani wa kukusanya pointi moja kila baada ya dakika 90 ipo kwenye mstari wa kushuka daraja.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.