WALTER Harson, Meneja wa Yanga amesema kuwa mchezo wao dhidi ya Singida Black Stars ulikuwa wenye ushindani mkubwa kutokana na mvua kubwa mchezo huo ulishindwa kumalizika huku wakiwashukuru mashabiki kwa kujitokeza kwa wingi kuwashangilia.
Ni Machi 24 Singida Black Stars waliwakaribisha Yanga katika mchezo wa kirafiki ambapo ulikuwa maalumu kwa ajili ya uzinduzi wa Uwanja wa Airtel.
Mpaka mpira unagota mwisho ubao ulikuwa unasoma Singida Black Stars 1-1 Yanga huku Jonathan Ikangalombo akiandika rekodi ya kuwa nyota wa kwanza kufunga bao ilikuwa dakika ya 19.
Kwa upande wa Singida Black Stars ni Marouf Tchakei ambaye aliweka usawa bao la Jonathan katika mchezo huo kipindi cha pili ambapo hali ya hewa bado ilikuwa sio rafiki kutokana na uwepo wa upepo na mvua.
Harison amesema: “Ni mchezo ambao ulikuwa na ushindani mkubwa unaona burudani ilikuwa inatolewa na mashabiki wengi walijitokeza kwa hilo tunawashukuru na tumeona namna uwanja ulivyo ikiwa ni maendeleo kwa mpira wetu kwa kuwa uwekezaji unazidi kuwa mkubwa.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.