TAIFA STARS KAMILI KUIKABILI MOROCCO KUWANIA KUFUZU KOMBE LA DUNIA

HEMED Morocco, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ameweka wazi kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo dhidi ya timu ya taifa ya Morocco ambao unatarajiwa kuchezwa leo Machi 25 2025 kwa wababe hao kuwania ushindi ndani ya uwanja.

Morocco amebainisha kuwa wanatambua ushindani ni mkubwa kwenye mchezo huo ila wapo tayari kupata matokeo chanya kwa kuwa kwenye mechi ambazo wanacheza ugenini wamekuwa na nguvu kupata matokeo.

Kocha huyo amesema: “Wachezaji wote wako vizuri, kwa ajili ya mchezo wetu na tunaamini kwamba tutapata matokeo ndani ya uwanja kwa kuwa hicho ni kitu ambacho tunakitafuta. Wachezaji  wananipa nguvu kuelekea kwenye mchezo wetu mara nyingi tumekuwa tukicheza ugenini tunakuwa na nguvu zaidi.”

Kuhusu hali ya hewa kocha huyo amebainisha kuwa hali ya hewa ya baridi Morocco ni baridi tofauti na hali ya hewa ya Bongo.

Saimon Msuva anasema ‘majina makubwa’ ya wachezaji wa Morocco hayawatishi wapo tayari kwa ushindani na lengo kubwa ni kupata matokeo mazuri.

Mechi ni saa 6:30 usiku wa kuamkia Machi 26 ambapo wababe hawa wanatarajiwa kuwa uwanjani kusaka ushindi ndani ya dakika 90.