UONGOZI wa Simba umebainisha kuwa tayari unaendelea na maandalizi ya mechi za ushindani zilizo mbele yao ikiwa ni mchezo wa hatua ya CRDB Federation Cup dhidi ya Big Man ambao unatarajiwa kuchezwa Machi 27 2025, Uwanja wa KMC Complex.
Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amebainisha kuwa wanatambua uwepo wa mechi zao zilizopo mbele jambo ambalo limewafanya waanze maandalizi huku akisema kuwa wapinzani wao Big Man wanatoka kwenye daraja dogo lakini jina lao linatisha kwa kuwa linamaanisha mtu mkubwa.
Mbali na mchezo wa CRDB Federation Cup Simba itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi dhidi ya Al Masry mchezo wa robo fainali Kombe la Shirikisho Afrika ambapo mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Aprili 2 2025 wataanzia Misri na kete ya mwisho itapigwa Aprili 9 2025.
Ahmed amesema kuwa mwalimu, Fadlu Davids anaendelea na mpango kazi kuelekea kwenye mechi hizo ambapo ameomba wacheze mechi za kirafiki kuwa fiti kuelekea mechi zijazo kwa kuwa walicheza muda mrefu hivyo jambo hilo linaendelea.
Miongoni mwa mchezo wa kirafiki ambao Simba walicheza ilikuwa dhidi ya KMC na walipata ushindi wa mabao 4-0.
Ahmed amesema: “Tunaendelea na maandalizi kuelekea mechi zetu mbili zilizopo mbele yetu ukiwa ni mchezo dhidi ya Big Man huu ni wa CRDB Federation Cup. Hii ni timu kutoka madaraja ya chini tunawaheshimu na jina lao linatisha kwani inamaanisha mtu mkubwa hivyo lazima tuchukue tahadhari zote tusifanye makosa yaliyopita.”.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.