WINGA wa kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids, Ellie Mpanzu ameweka wazi kuwa bado hajafikia ubora wake kwa asilimia 100 kwenye mechi za ushindani hivyo kwa maana hiyo gari bado halijawaka.
Hivyo licha yakuwa kwenye mwendelezo katika mechi ambazo anacheza bado chuma hakijapata moto kufikia makali ambayo anayo kutokana na uwezo wake katika mechi za ushindani.
Nyota huyo ameingia moja kwa moja kikosi cha kwanza ikiwa ni ingizo jipya katika dirisha dogo ndani ligi ambayo inadhaminiwa na NBC katupia mabao matatu na Simba ni mabao 52 imetupia jumla.
Sio kufunga tu nyota huyo anatengeneza pasi za mabao pia akiwa nazo mbili hivyo amehusika kwenye mabao matano kati ya 52 yaliyofungwa na Simba na kinara kwenye chati ya utupiaji ni Jean Ahoua mwenye mabao 12 na yote kafunga akitumia mguu wa kulia.
Mpanzu rekodi zinaonyesha kuwa amecheza mechi 10 na kukomba dakika 784 ana wastani wa kuwa na hatari kila baada ya dakika 156.
Mpanzu amesema: “Nimekuja katikati ya msimu nab ado sijafikia ule ubora kwa asilimia 80 ambao ninautaka hivyo ninazidi kupambana kufikia 100 kikubwa ni ushirikiano. Nina amini tutafanya vizuri kutokana kila mchezaji kuwa tayari.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.