HII HAPA MITAMBO YA MABAO KUTOKA KARIAKOO

NDANI ya Ligi namba nne kwa ubora Afrika kuna mashine za kazi eneo la ushambuliaji ambazo zimekuwa kwenye mwendo mzuri kutoka kikosi cha Simba ambacho kinanolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Vita sio nyepesi kwenye eneo la ushambuliaji ambapo mabingwa watetezi Yanga wao pointi zao kibindoni ambazo ni 58 ni saw ana idadi ya mabao ambayo wamefunga huku wakifuatiwa na Simba yenye mabao 52 kibindoni.
Timu zote zimeshuka uwanjani kwenye mechi 22 ndani ya msimu wa 2024/25 katika msako wa pointi tatu muhimu huku kwenye mzunguko wa kwanza walipokutana wababe hawa ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 0-1 Yanga.

Mzunguko wa pili ngoma ilitarajiwa kuchezwa Machi 8 2025 ikayeyuka baada ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania kutangaza kuwa wataupangia mchezo huo tarehe nyingine ambayo kwa sasa inasubiriwa na mashabiki na timu hizo mbili.

Kwenye eneo la kufunga, Yanga imekuwa na kasi kubwa ikiwapoteza watani zao wa jadi Simba kwa tofauti ya mabao sita ambapo wote wamecheza jumla ya mechi 22 ambazo ni dakika 1,980 huku Yanga ikiwa na wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 34 na Simba wakiwa na wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 38.

Jean Ahoua ni namba moja kwa utupiaji akiwa ametupia mabao 12 na ametoa pasi 7 za mabao, yupo zake ndani ya kikosi cha Simba kilicho nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi huku Steven Mukwala akiwa ametupia mabao 9 na ametoa pasi 2 za mabao.

Kutoka Yanga kuna wakali wawili ambaoni washambuliaji wote wametupia mabao 10 kila mmoja, Dube ambaye katoa pasi 7 za mabao zinamfanya ahusike kwenye mabao 17 na Clement Mzize ambaye katoa pasi nne za mabao zinamfanya ahusike kwenye mabao 14.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.