WALTER Harison, Meneja wa Yanga amesema kuwa Wananchi watapata burudani ambayo waliikosa kwa muda kutokana na mchezo wa kirafiki dhidi ya Singida Black Stars unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Airtel.
Yanga inatarajiwa kushuka uwanjani Machi 24 2025 kwa ajili ya mchezo wa kirafiki amba oni maalumu kwa ajili ya uzinduzi wa uwanja mpya wa Singida Black Stars yenye maskani yake Singida kwenye mechi za nyumbani kabla ya uwanja mpya ni Uwanja wa Liti ulikuwa unatumika.
Machi 23 kikosi cha Yanga kinchonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi kilianza safari kutoka Dar kuelekea Dodoma kwa SGR kisha wakachukua basi mpaka Singida ambapo tayari kwa sasa wapo hapo kwa maandalizi ya mwisho ya mchezo huo unaosubiriwa kwa shauku kubwa.
Harison amesema kuwa safari yao ilikuwa nzuri na wanatambua wanakwenda kukabiliana na timu yenye ushindani mkubwa jambo ambalo linatoa burudani kwa timu zote mbili uwanjani hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi kushuhudia mchezo huo.
“Wananchi watapata burudani ambayo waliikosa kwa muda mrefu utakumbuka kwamba mzunguko wa kwanza hatukucheza hapa mchezo wetu wa ligi hivyo mchezo wetu wa uzinduzi wa uwanja ni maalumu kuwapa burudani wajitokeze.
“Wachezaji wapo tayari kwa mchezo na wanatambua umuhimu wa mchezo huu hasa ukizingatia ni kwenye uzinduzi, Singida Black Stars sio timu yakubeza tunatambua uwezo wake hivyo tutaingia kwa tahadhari ili kupata burudani na matokeo mazuri.”
Miongoni mwa wachezaji wa Yanga waliopo kwenye kikosi ni Jonas Mkude, Maxi Nzengeli, Sure Boy, Farid Mussa, Dennis Nkane.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.