NAIBU HAMIS MWINJUMA AZINDUA UWANJA, REKODI YAANDIKWA

NAIBU Waziri Utamaduni Sanaa na Michezo Hamis  Mwinjuma, maarufu kwa jina la FA rasmi amezindua Uwanja wa Airtel, Singida ambao utatumiwa na timu hiyo kwa mechi za ushindani.

 FA kwenye uzinduzi huo amepiga bonge moja ya penati ambayo ilimshinda mlinda mlango namba moja wa Singida Black Stars, Metacha Mnata.

Ilikuwa ni kwa mguu wake wa kulia ambapo alipiga penati hiyo kuashiria uzinduzi rasmi wa uwanja huo ambao umejengwa kwa udhamini mkubwa wa kampuni ya Airtel.

Mashabiki wamejitokeza kwa wingi kwenye uzinduzi huo ambapo kuna mchezo wa kirafiki dhidi ya Yanga.

Kwenye mchezo huo tayari rekodi imeandikwa kwa mshambuliaji Jonathan Ikangalombo kufunga bao la kwanza kwenye uwanja huo mpya dakika ya 19 akimtungua Mnata.

Hiki hapa kikosi cha Singida Black Stars kwenye mchezo dhidi ya Yanga:-

Metacha Mnata, Mkumbo, Malonga, Assinki, Trabi, Damaro, Keyekeh, Pokou, Adebayor, Bada, Sowah na wachezaji wa akiba ni Benedict Haule, Manyama, Kennedy, Khalid, Nashon, Edmund, Mwanuke, Imoro,Lyanga, Mpepo, Chukwu, Gadiel, Rashid.

Kikosi cha Yanga

Khomeiny, Kibwana Shomary, Nickson Kibabage, Aziz Andambwile, Boka, Jonas Mkude, Maxi Nzengeli, Sure Boy, Pacome, Ikanga lombo, Sheikhan huku wachezaji wa akiba ni Aboutwalib Mshery, Israel Mwenda, Farid Musa na Dennis Nkane.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.