MBEYA KWANZA HAWAPOI HUKO, KAZI INAENDELEA

KAZI inaendelea kwa Mbeya Kwanza ambao hawapoi kabisa kwani baada ya ushindi kwenye mchezo wao uliopita wa NBC Championship dhidi ya Polisi Tanzania sasa hesabu kubwa ni kwenye mchezo ujao dhidi ya Transit Camp.

Katika mchezo huo Mbeya Kwanza iliyo nafasi ya 6 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 42 baada ya mechi 24 za ushindani ilikomba pointi tatu mazima mbele ya Polisi Tanzania iliyo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 28 nayo imecheza mechi 24.

Lyin Essau, Ofisa Habari wa Mbeya Kwanza ameweka wazi kuwa kazi kubwa inayofanyika na wachezaji kwenye kutafuta matokeo wakitumia mbinu wanazopewa na benchi la ufundi zinawapa nguvu yakupata matokeo mazuri kwenye ligi ambayo ina ushindani mkubwa.

“Tunaanza mazoezi kesho kwa ajili ya kujiandaa na mchezo ujao dhidi ya Transit Camp nah ii ni baada ya kutoka kucheza mchezo wetu dhidi ya Polisi Tanzania ambao tuliibuka na ushindi wa bao 1-0.

“Kwenye mchezo wetu huo uliokuwa na ushindani mkubwa bao pekee la ushindi ambalo lilitupa pointi tatu muhimu kwenye uwanja ndani ya dakika 90 lilifungwa na Baraka Mwangosi hivyo kwa sasa tunakwenda kuanza maandalizi kuelekea mchezo wetu ujao, mashabiki wazidi kuwa pamoja nasi.”

Wapinzani wa Mbeya Kwanza, Transit Camp kwenye msimamo wapo nafasi ya 15 kibindoni wana pointi 11 huku vinara wakiwa ni Mtibwa Sugar wenye jumla ya pointi 57 baada ya mechi 24.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.