BODABODA WA KARIAKOO WANUFAIKA NA UJIO WA MERIDIANBET

Jumamosi tamu kabisa ya wewe kuondoka na pesa pale Meridianbet imefika, huku wakali hao wa ubashiri leo hii wao wakiamua kurejesha kidogo wanachokipata na safafri hii ilikuwa ni pale Kariakoo ambapo wametoa reflectors na helmet.

Katika jitihada za kuimarisha usalama barabarani, Meridianbet imefanya tukio la kugawa helmet na reflectors kwa madereva wa boda boda katika maeneo ya Kariakoo na Fire.

Tukio hili ni sehemu ya dhamira ya Meridianbet ya kusaidia jamii na kuhakikisha usalama wa madereva pamoja na abiria wao. Madereva wa boda boda ni sehemu muhimu ya mfumo wa usafirishaji jijini Dar es Salaam, na kupitia msaada huu, kampuni inalenga kupunguza ajali na kuongeza ufanisi wa safari za kila siku.

Reflectors hizi na helmet zitawasaidia madereva wa bodaboda kuonekana na madereva wengine na kuwawezesha kuonekana kwa urahisi, hivyo kupunguza ajali.

Bashiri na Meridianbet mechi za kufuzu kombe la Dunia ushinde zaidi ya mamilioni. Pia cheza michezo ya Kasino ya mtandaoni kama vile, Aviator, Keno, Poker, Roullette, Keno, na mingine kibao.

“Usalama barabarani ni jukumu la kila mmoja wetu. Tunajivunia kuwa sehemu ya suluhisho kwa kusaidia madereva wa boda boda kupata vifaa muhimu vinavyoongeza usalama wao wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.” Mwakilishi wa Meridianbet alisema.

Meridianbet inawahamasisha madereva wote wa boda boda kutumia helmet na reflectors kila mara wanapokuwa barabarani ili kulinda maisha yao na ya wengine.

Kwa msaada huu, Meridianbet inathibitisha kwa mara nyingine tena dhamira yake ya kuleta maendeleo ya kijamii kupitia kampeni za usalama na ustawi wa jamii.

Meridianbet imesema kuwa inatmbua kuwa madereva wa bodaboda wanachangia sana katika uchumi wa nchi, na ni jukumu lao kuhakikisha wanapata mazingira salama ya kufanya kazi zao.