NYOTA MPYA YANGA BALAA LAKE SIO LA KITOTO

MILOUD Hamdi, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa ingizo jipya ndani ya Yanga ambaye ni mshambuliaji Jonathan Ikangalombo ana spidi kubwa akiwa uwanjani jambo ambalo ni faida kwa timu kwenye mechi za ushindani.

Kocha huyo ameweka wazi kuwa mshambuliaji huyo alikuwa hachezi kwenye mechi zilizopita kwa kuwa hakuwa fiti kwa asilimia kubwa jambo ambalo lilifanya asionekane uwanjani katika mechi za ushindani licha ya uwezo alionao.

“Nilisema awali kwamba Ikangalombo ni mchezaji mzuri lakini alikuwa haonekani uwanjani kwa kuwa alikuwa bado hayupo fiti, kwenye mechi alizocheza nina amini kila mmoja ameona, ana spidi, nguvu na uwezo wakufuata maelekezo akiwa uwanjani.”

Machi 12 dhidi ya Coastal Union mchezo wa CRDB Federation Cup ulikuwa ni mchezo wake wa pili akiwa na uzi wa Yanga alianzia benchi na alipata nafasi ya kucheza na ubao ulisoma Yanga 3-1 Coastal Union.

Februari 23 2025 dhidi ya Pamba Jiji mchezo uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba na mwisho ubao ukasoma Pamba Jiji 0-3 Yanga kwa mabao mawili ya Aziz Ki aliyechaguliwa kuwa mchezaji bora na bao moja likifungwa na Boka ulikuwa ni mchezo wake wa kwanza kwenye ligi akianzia benchi.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.