WACHEZAJI SIMBA WABEBESHA ZIGO LA LAWAMA

KOCHA wa Simba Queens, Yassif Basigi amelia na wachezaji wake kushindwa kutumia nafasi za wazi ambazo walizipata kwenye mchezo wa Kariakoo Dabi Ligi ya Wanawake ndani ya dakika 90 ambazo walizipata.

Kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC Complex Machi 18 2025 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba Queens 0-1 Yanga Princess ambapo katika dakika 45 za mwanzo timu zote mbili zilitoshana nguvu kwa kila mmoja kukwama kupata bao kwenye mchezo huo.

Upepo ulibadilika kipindi cha pili katika dakika 15 za mwanzo Yanga Princess walipata nafasi ya dhahabu dakika ya 46 kupitia kwa Jeannine Mukandayisenga dakika ya 49 lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huo.

Jitihada za Simba Queens kwenye mchezo huo kupata bao la kuweka usawa hazikuleta matunda licha ya nafasi ambazo walikuwa wakizipata mpaka dakika 90 zinakamilika ngoma ilikuwa ni nzito kwao.

Kocha huyo amesema kuwa walikuwa na nafasi za kufunga kwenye mchezo hasa kipindi cha kwanza na kipindi cha pili ilikuwa hivyo lakini walikwama kupata matokeo jambo ambalo watalifanyia kazi kwenye mechi zijazo.

“Tulikuwa na nafasi kufunga kwenye mchezo wetu na ilikuwa hivyo kuanzia kipindi cha kwanza nafasi za wazi kabisa lakini wachezaji walishindwa kufunga, huu ni mpira na matokeo yametokea tumepoteza ni muda wetu kufanyia kazi makosa kwa ajili ya mechi zinazofuata.”

Safu ya ushambuliaji ya Simba Queens inaongozwa na Jenrix Shikangwa ambaye ni chaguo la kwanza na kipa ni Wilfrida Ceda ambaye alitunguliwa bao hilo kwenye Kariakoo Dabi.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.